Apple yatishia kuiondoa Twitter kwenye App Store

0
54

Mfanyabiashara Elon Musk ambaye ni mmiliki mpya wa mtandao wa Twitter ameishutumu Kampuni ya Apple kwa kutishia kuiondoa Twitter kwenye programu zake bila kutoa sababu.

Mmiliki huyo pia amedai kuwa tayari kampuni nyingi ikiwemo iPhone zimesitisha kutangaza kwenye mtandao huo kutokana na mipango yake katika kudhibiti maudhui kwenye mtandao huo.

“Apple pia imetishia kuiondoa Twitter kwenye ‘App Store’ lakini haijatuambia ni kwa nini,” ameandika Musk.

Hata hivyo, Apple bado haijatoa majibu kutokana na shutuma hizo za Musk ambaye anakiri mapato ya Twitter kushuka kwa kiwango kikubwa huku akiwalaumu wanaharakati kwa madai kuwa wanawashinikiza watangazaji wajiondoe.

Mwanamke akamatwa akijaribu kupenyeza bangi kwa mumewe aliyeko gerezani

Wiki iliyopita Musk alitangaza msamaha kwa akaunti zilizofungiwa ikiwemo aliyekuwa mshauri wa zamani wa Donald Trump, Steve Bannon.

Aidha, tayari amerejesha akaunti ya Rais Mstaafu wa Marekani, Donald Trump ingawa, Rais huyo bado hajaitumia tangu aruhusiwe kurudi kwenye mtandao huo.

Send this to a friend