Arusha: Kituo maalum cha polisi cha watalii chawahakikishia usalama wageni

0
38

Kituo cha Polisi maalumu kwa ajili ya kuhudumia watalii na wanadiplomasia mkoani Arusha kinatarajiwa kuimarisha ulinzi na usalama kwa wageni watakaofika mkoani humo kufuatia uzinduzi wa filamu ya Tanzania: The Royal Tour.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Justine Masejo amesema askari kwenye vituo hivyo wamewapatiwa mafunzo ndani na nje ya nchi juu ya namna bora ya kuhudumia watalii.

Ameeleza kuwa katika mkoa huo ambao ni kotovu cha utalii Tanzania kuna magari maalumu ambayo hutumiwa na kituo hicho kwa ajili ya doria mbalimbali ikiwemo kwenye vivutio vya utalii, hoteli za kitalii pamoja na maeneo mengine ambayo wageni hupenda kutembelea.

Sambamba na hilo amesema kuwa kuna vituo vidogo vya Polisi vilivyopo katika wilaya ya Arumeru, Monduli, Longido, na Karatu ambapo magari ya utalii hufika kwa ajili ya kupata taarifa za kitalii pamoja na ukaguzi wa usalama wa magari hayo.

Send this to a friend