Arusha mawe kituo cha polisi akiwa amelewa

0
38

Maafisa wa polisi katika eneo la Solai, Kaunti ya Nakuru nchini Kenya, wamemkamata mwanaume mmoja anayejulikana kwa jina la Dennis Kibet kwa kosa la kurusha mawe katika kituo cha polisi na kumjeruhi Afisa wa Polisi, akiwa amelewa.

Kulingana na ripoti ya Polisi, mwanaume huyo alimshambulia afisa huyo wa Polisi, Eliud Misiko kwa mawe wakati akirejea kazini baada ya mapumziko ya mchana na kujeruhiwa bega lake.

Ripoti hiyo inaeleza kwamba mtuhumiwa alipohojiwa kwanini amefanya tukio hilo alidai kuwa, alitaka aone jinsi atakavyojihisi endapo akirusha mawe katika kituo cha polisi.

Hata hivyo mshtakiwa mbali na kukamatwa kwa kosa la kushambulia kituo cha polisi na kumjeruhi Afisa wa polisi, alikutwa na roli kumi za bangi na kuongeza idadi zaidi ya makosa yake.

Mwanaume huyo ambaye alionekana kutokerwa hata kidogo na matendo yake, kwa sasa yuko chini ya ulinzi wa polisi kwa mahojiano zaidi.

Send this to a friend