Arusha: Wananchi washambuliwa na mawe kutoka kusikojulikana

0
41

Wakazi wa Kijiji cha Kiwawa Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha wameingia kwenye taharuki baada ya mawe kurushwa kwenye maeneo yao na watu wasiojulikana.

Wananchi wamedai mawe hayo hayajulikani yanapotokea na yamesababisha  uharibifu mkubwa wa nyumba na baadhi ya wananchi wajeruhiwa, hivyo kuwalazimu kutumia ndoo ili kujihami vichwa vyao.

Kwa mujibu wa wakazi wa eno hilo wamedai mawe yamekuwa yakirushwa kwa zaidi ya wiki moja kuanzia saa 12:00 jioni hadi saa 4: 00 usiku na kuanza tena saa 11:00 alfajiri.

“Serikali haiamini uchawi, tumeshatoa taarifa kituo cha polisi cha Usa River lakini hatujapata msaada, wametuambia tuunde vikosi shirikishi vya ulinzi na kufanya doria na tumefanya hivyo, lakini hatujafanikiwa kumkamata mhusika,” amedai mkazi wa eneo hilo, Gilbert Nnko.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa Kijiji cha Kiwawa, Ernest Pallangyo amesema hali hiyo imesababisha taharuki na hofu kwa wananchi wa kijiji hicho, na sasa amewaelekeza wananchi kuhakikisha watoto wanakaa ndani na watu wazima kuchukua tahadhari wanapokuwa nje ili kuepuka madhara yanayotokana na mawe hayo.

Send this to a friend