ARVs zatumika kunenepesha kuku na nguruwe

0
81

Mamlaka ya Taifa ya Udhibiti wa Dawa nchini Uganda (NDA) imekiri kutambua matumizi ya dawa za kupunguza makali ya Virusi vya UKIMWI (VVU) zilitumika kunenepesha mifugo.

Inspekta Mkuu NDA, Amos Atumanya ameliambia Bunge la Uganda hivi karibuni kwamba walijua dawa hizo zilitumika kuwatibu kuku na nguruwe mwaka 2014 lakini hawakutoa onyo kwa umma.

Atumanya amesema iwapo kuna hatari yoyote ya kiafya ingeonya umma huku akieleza kuwa kazi ya mamlaka hiyo ni kudhibiti matumizi ya dawa na sio chakula wala mifugo.

Mchungaji aamriwa kumrudishiwa muumini fedha alizodai ni fungu la 10

Aidha, ripoti ya hivi karibuni kutoka Chuo Kikuu Makerere iligundua zaidi ya theluthi moja ya kuku na asilimia 50 ya nguruwe waliofanyiwa vipimo walikuwa na chembechembe za dawa hizo za kukabiliana na ugonjwa huo.

Mmoja wa watafiti chuoni hapo alisema nguruwe na kuku ambao hupewa dawa za kupunguza makali ya VVU hukua haraka na kunenepa hivyo huuzwa kwa haraka.

Send this to a friend