Asakwa kwa kumfumua mgonjwa kidonda baada ya kushindwa kulipia

0
45

Mhudumu wa afya ambaye hajafahamika jina lake wala kituo cha kazi amedaiwa kufumua nyuzi kwenye kidonda cha mgonjwa kwa madai mgonjwa huyo alishindwa kulipia gharama za matibabu.

Kufuatia tukio hilo Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeeleza kupokea kwa masikitiko na kusema “Ikiwa hili limetokea nchini Tanzania, basi ni ukiukwaji mkubwa wa huduma za kitabibu.”

Kufuatia tukio hilo, wizara imeomba yeyote mwenye taarifa za wapi tukio lilipotokea au kituo gani awasilishe mara moja kwa namba ya huduma kwa mteja 199 ya wizara ya afya au atume ujumbe mfupi kwenye namba ya Waziri wa Afya ya 0734124191.

Send this to a friend