Ashikiliwa kwa kudaiwa kumuua rafiki yake kisa wivu wa mapenzi

0
33

Jeshi la Polisi linamshikilia Amos Mwita (17) mkazi wa Bugarika Bendera Tatu, Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza kwa tuhuma za mauaji ya Daniel Kisire (18) kwa sababu za wivu wa mapenzi.

Oktoba 24, mwaka huu, mtuhumiwa huyo anadaiwa kumuua Kisire kwa kumchoma kisu shingoni nyumbani kwa bibi yake baada ya kuzuka ugomvi uliotokana na wivu wa mapenzi na kusababisha kifo chake.

Inadaiwa Kisire na Mwita ni majirani, ambapo marehemu Kisire alimtaka kimapenzi binti aitwaye Latifa Chombo (14), mkulima na mkazi wa Bugarika ambaye alimkatalia na baadaye binti huyo alianza mahusiano na Mwita ambaye ni rafiki wa Kisire.

“Mara baada ya mtuhumiwa kufanya tukio hilo alitoroka na kwenda kusikojulikana, ambapo Oktoba 25, 2024, Jeshi la Polisi lilifanikiwa kumkamata akiwa mafichoni nyumbani kwa rafiki yake huko Bugarika,” imeeleza taarifa ya Polisi.

Jeshi la Polisi limesema linaendelea na upelelezi wa tukio hilo na mtuhumiwa atafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.

Send this to a friend