Ashikiliwa kwa tuhuma za kumbaka bibi wa miaka 73

0
35

Mwanaume mwenye umri wa miaka 45 amekamatwa kwa tuhuma za kumbaka mwanamke mwenye umri wa miaka 73 katika kaunti ya Tharaka Nithi.

Kulingana na Kamanda wa Polisi wa Kaunti hiyo, Zacchaeus Ngeno, tukio hilo lilitokea katika eneo la KK Ndagani, katika Eneo Bunge la Chuka Igambang’ombe.

Kwa mujibu wa uchunguzi wa awali, mtuhumiwa, aliyejulikana kama James Mutembei, alitembelea nyumbani kwa mwathiriwa na kumkuta akiwa na mume wake, kisha akamshawishi mume wa mwathiriwa kuwa mama yake anamuita, hali iliyomfanya mume wa mwathiriwa kuondoka nyumbani.

Hata hivyo, mtuhumiwa alirudi nyumbani kwa mwathiriwa akiwa peke yake kisha kumbaka bibi huyo. Polisi wamefanikiwa kumkamata mtuhumiwa na kumpeleka katika kituo cha polisi cha Chuka, ambako anashikiliwa akisubiri kufikishwa mahakamani Jumanne.

Polisi wamesema wanaendelea na uchunguzi zaidi kuhusu tukio hilo ambalo limezua hisia kali miongoni mwa wakazi wa eneo hilo, huku wakiitaka jamii kuwa macho na kutoa ushirikiano katika kuimarisha usalama.

Send this to a friend