Ashikiliwa kwa kumbaka na kumuua mtoto wa chekechea wakati akienda shuleni

0
31

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kusini Unguja linamshikilia Maulid Hassan Maulid (18) mkazi wa Mwera Pongwe katika Wilaya ya Kati mkoani humo kwa kosa la kumwingilia kimwili na kusababisha kifo cha mtoto Khadija Mhoda mwenye umri wa miaka 6 na mwanafunzi wa chekechea.

Taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi imeeleza kuwa Novemba 14, 2024 majira ya saa 1 asubuhi, mtoto huyo aliondoka nyumbani kwao kuelekea shuleni ambapo mama yake alimkabidhi kwa kijana mmoja ili ampeleke shuleni.

“Yule kijana hakumfikisha shuleni baada ya kuwaona wanafunzi wengine akamuacha aongozane naye.

Majira ya saa 7 mchana hakurudi nyumbani kama ilivyo kawaida yake, jambo ambalo lilimpa wasiwasi mama yake na alipoulizia shuleni akajulishwa kuwa binti yake hakufika shuleni ndipo alipopeleka taarifa Kituo cha Polisi Dunga,” imesema taarifa.

Imeelezwa kuwa majira ya saa 10 jioni huko Mwera Vichaka Mabundi, mwili wa binti huyo ulionekana kwenye jengo ambalo halijakamilika akiwa amefariki dunia.

Jeshi la Polisi limesema baada ya kufanya upelelezi kwa kushirikiana na wananchi likafanikiwa kumkata mtuhumiwa ambaye alibainika kuwa ndiye aliyemkamata binti huyo wakati anaenda shule, huku akimziba mdomo na kumuingiza kwenye boma na kumfanyia ukatili huo.

Send this to a friend