
Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro linamshikilia mwanaume mmoja (26) mkazi wa Kijiji cha Kirwa wilayani Rombo kwa kosa la kumuua mtoto Rosemary Mathias (06), mwanafunzi wa darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Mahaheni kwa kumkata shingo na kutenganisha kiwiliwili na kichwa Machi 15, 2025.
Taarifa ya Jeshi la Polisi imeeleza kuwa siku ya tukio mtuhumiwa alirudi kwao akitokea matembezini akiwa ameshika panga mkononi na kuwakuta watoto wakiwa wanacheza, ambapo katika hali ya kushangaza alimkamata binti huyo na kuteketeza ukatili huo.
“Chanzo cha tukio hili bado kinachunguzwa, taratibu za kiuchunguzi zitakapokamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakama, ” imesema taarifa hiyo.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Huruma wilayani Rombo kusubiri uchunguzi na taratibu zingine za mazishi.