Ashikiliwa kwa kumuua baba mkwe wake wakati wakisuluhisha ndoa yake

0
38

Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro linamshikilia Deogratias Mbuya (40) kwa tuhuma za kumuua baba mkwe wake pamoja na kumjeruhi mama mkwe wake kwa panga baada ya kutokea kwa mtafaruko kwenye kikao ambacho kililenga kupatanisha ndoa ya mtuhumiwa huyo.

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Simon Maigwa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo siku ya Jumatano majira ya saa 7 mchana nyumbani kwa baba mkwe huyo, Tibrus Mneney (72).

“Chanzo cha tukio hilo ni ugomvi uliozuka kwenye kwenye kikao cha usuluhishi wa mgogo kati ya mtuhumiwa na mke wake unaohusu wivu wa mapenzi,” amesema Kamanda.

Kamanda Maigwa ameeleza kuwa baada ya usuluhishi kugonga mwamba, myuhumiwa alianza kufanya vurugu na kumjeruhi mama mkwe wake, Bertha Mneney (58) ndipo baba mkwe wake alipoingilia kati kumuokoa mke wake na mtuhumiwa huyo kuanza kumshambulia kwa kitu chenye nsha kali katika sehemu zake za mwili hali iliyopelekea kuvuja damu nyingi na kupoteza maisha.

Amesema baada ya kutekeleza tukio hilo, mtuhumiwa alitoroka na baada ya msako mkali wa polisi kwa kushirikiana na wananchi walifanikiwa kumpata akiwa amejificha kwenye jengo tupu, na kwasasa amelazwa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya KCMC kwa uchunguzi wa kiafya.

Send this to a friend