Ashikiliwa kwa tuhuha za mauaji ya watoto watatu wa familia moja

0
34

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia Doto Lubongeja mkazi wa Madundasi wilayani Mbarali, kwa tuhuma za mauaji ya watoto watatu wa familia moja kwa kuwanyonga shingo, kisha kuiba ng’ombe 15.

Watoto hao waliouawa ni Petro Amosi (08), Samu Amosi (06) na Nkamba Amosi (04) wote wa familia moja ambao walikuwa wakichunga ng’ombe katika eneo jirani na nyumba wanayoishi.

Tukio hilo limetokea Januari 15, 2026 katika Kijiji cha Matundasi, Kata ya Matundasi, Wilaya ya Chunya, Mkoa wa Mbeya ambapo imeelezwa kuwa baada ya wizi huo mtuhumiwa alizificha nyumbani kwa mjomba wake aitwaye Masoda Kurwa anayeishi Kijiji cha Madundasi ‘B’ na kuanza kutafuta mteja ambapo alifanikiwa kuwauza na kupata kiasi cha shilingi milioni 5.1.

“Kufuatia tukio hilo, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kupitia askari wa kuchunguza matukio ya mauaji, walianza msako mkali na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa pamoja na mtuhumiwa mwingine aitwaye Masoda Kurwa ambaye walishirikiana kuuza ng’ombe hao,” imeeleza taarifa ya polisi.

Aidha, polisi wamesema uchunguzi wa awali umebaini chanzo cha tukio hilo ni tamaa ya kujipatia mali kwa njia isiyo halali.

Send this to a friend