Ashikiliwa kwa tuhuma za kuvunja na kuiba pesa benki

0
39

Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limesema limemkamata Denis Ogesa (28) mkazi wa Nairobi nchini Kenya, kwa tuhuma za kuvunja na kuingia katika tawi la benki ya Azania iliyopo katika mji wa Namanga wilayani Longido na kisha kuiba fedha.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Justine Masejo amesema mtuhumiwa huyo alitenda tukio hilo Januari 14, 2026 muda wa saa 6:40 usiku.

SACP Masejo amebainisha kuwa wakati mtuhumiwa huyo akiendelea kutekeleza tukio hilo la kihalifu katika benki hiyo, alikamatwa akiwa tayari na fedha za Tanzania zenye thamani ya TZS 91,280,000 na fedha za Kenya zenye thamani ya shilingi 288,700.

Jeshi la Polisi mkoani humo limesema linakamilisha uchunguzi kuhusu watu alioshirikiana nao ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa.

Send this to a friend