Ashikiliwa kwa tuhuma za kuwanajisi watoto wake mapacha

0
50

Jeshi la Polisi mkoani Morogoro linamshikilia Hamad Kapera (20) mkazi wa Kilosa mkoani Morogoro kwa tuhuma za kuwanajisi watoto wake mapacha wenye umri wa miaka miwili na kuwaambukiza magonjwa ya zinaa.

Imeelezwa kuwa, tukio hilo la kikatili lilitokea Mei 21 wakati mama yao alipokwenda shambani na kuwaacha watoto nyumbani wakiwa na baba yao na ndipo ukatili huo ulipofanyika.

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Alex Mkama amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa mwanaume huyo anashikiliwa pamoja na mke wake kwa kosa la kukataa kutoa ushahidi.

Hata hivyo, imeelezwa kuwa mama wa watoto hao ambaye jina lake limehifadhiwa, alifika ofisini kwa Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Shaka Hamdu Shaka kuomba mume wake asamehewe ili waendelee kuwalea watoto wao.

“Nilikuwa shamba niliota watoto wanaingiliwa, ila sikujua ni nani, nikamweleza mwenzangu tukarudi nyumbani, nikawaogesha watoto wangu ila nikaona kuna utofauti. Nikajiuliza wameingiliwa ama ni magonjwa, nikaambiwa huenda ni magonjwa iwapo wangeingiliwa hawa watoto wa miaka miwili wasingeweza kutembea,” Mkuu wa Wilaya alinukuu maneno ya mama huyo.

Shaka amesema mama huyo aliamua kuwapeleka hospitali baada ya hali hiyo, nak u bainika kuwa watoto hao mapacha wameingiliwa na ndipo polisi walipoanza uchunguzi kwa kufanya mahojiano na mwanamke huyo kisha kumshikilia mume wake, kisha mama aliamua kwenda kwa Mkuu wa Wilaya kumuomba mumewe aachiwe.

Send this to a friend