Ashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kujifanya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya

0
15

Jeshi la Polisi mkoani Mbeya linamshikilia Warren Max Mwinuka (20) mkazi wa Makondeko Mbeya Mjini kwa tuhuma za kujifanya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera.

Mtuhumiwa huyo anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kutumia akaunti ya mtandao wa kijamii wa Instagram kwa jina la ‘juma_homera’

Inadaiwa kuwa mtuhumiwa alikuwa akitumia akaunti hiyo kuwahadaa watu kwa kujifanya ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya na kutoa namba ya simu ili wananchi waweze kutoa, kupeleka kero na shida mbalimbali kwake.

Mnamo Juni 07 mwaka huu mtuhumiwa alikamatwa majira ya saa 08:00 mchana huko maeneo ya Mama John Jijini Mbeya.

Meya Mwanza akanusha wananchi wa milimani kuondolewa

Jeshi la Polisi limesema kuwa upelelezi wa shauri hilo unaendelea na mara baada ya kukamilika atafikishwa mahakamani.

Send this to a friend