Ashitakiwa kwa kujifanya Rais Samia Mtandaoni

0
39

Kijana Nickson Mfoi (20) mkazi wa jiji la Mwanza amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi kwa tuhuma za kujifanya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan mtandaoni.

Akisoma shitaka hilo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Richard Kabate Wakili wa Serikali, Ashura Mnzava amesema Septemba 22, 2021 mshtakiwa alijiwasilisha mtandaoni kama Rais Samia Suluhu Hassan kwa nia ya ulaghai na udanganyifu, jambo ambalo ni kinyume na sheria.

Aidha, katika shitaka la pili mshitakiwa amekutwa akimiliki na kutumia laini ya simu iliyo katika umiliki wa mtu mwingine bila kutoa taarifa kwa mtoa huduma.

Mnzava amesema upelelezi wa kesi hiyo tayari umekamilika, na kuomba tarehe ya kumsomea mshitakiwa maelezo ya awali.

Hata hivyo mshitakiwa amerejeshwa mahabusu baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ya kupeleka mdhamini mwenye kazi inayoaminika.

Send this to a friend