Asilimia 10 ya Watanzania wana Kisukari

0
39

Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Kinga, Dk. Omary Ubuguyu amebainisha kuwa kati ya Watanzania milioni 60, zaidi ya milioni 5.7 (takribani asilimia 10) wanusumbuliwa na ugonjwa wa Kisukari.

Aliyasema hayo jijini Dodoma katika uzinduzi wa mpango wa kuzuia ulemavu wa kutoona unaoweza kusababishwa na madhara ya kisukari kwenye macho.

“Tanzania inakadiriwa kuwa na takribani asilimia 5.7 ya watu wenye umri wa miaka kati ya 20 na 79 wana Kisukari. Utafiti uliofanyika nchini unaonesha asillimia 35 ya wenye Kisukari wana madhara ya ugonjwa huo kwenye macho na asilimia moja yao, hupata ugonjwa wa kutoona au kuona hafifu,” amesema.

Aidha, ameeleza kuwa kuna taratibu nyingi za kuzuia ulemavu wa kutoona unaosababishwa na kisukari kwenye retina ikiwa ni pamoja na kuanza uchunguzi mapema kwa walio na kisukari pamoja na kuzingatia tiba na ushauri wa wataalamu ikiwemo kubadili mtindo wa maisha.

Send this to a friend