Asilimia 24 ya Watanzania hawajui kusoma na kuandika

0
56

Kwa mujibu wa ripoti mwaka 2020/21 ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) asilimia 76 ya Watanzania wanajua kusoma, kuandika na kufanya hesabu rahisi (simple arithmetic calculations), ikiwa ni ongezeko kutoka asilimia 69.8 mwaka 2014/15.

Mkoa wa Dar es Salaam unaongoza kwa kuwa na watu wengi wanaojua kusoma na kuandika ambao ni asilimia 94, huku watu wanaoishi vijijini kwa upande wa Tanzania Bara wanaojua kusoma na kuandika wakiwa ni asilimia 69.7.

Katika takwimu hizo NBS imeeleza kuwa wanaume ndio wanaongoza kwa kujua kusoma, kuandika na kufanya hesabu rahisi ikilinganishwa na wanawake.

Serikali yachunguza shule inayodaiwa kufundisha wanafunzi kulawiti

Kuongezeka kwa idadi ya wanaojua kusoma na kuandika ni matokeo ya jitihada za Serikali na wadau wa elimu kuhakikisha kuwa kiwango cha ujinga, kama moja ya maadui wa Taifa kinapunguzwa.

Kwa sasa Tanzania inatumia mfumo wa 2-7-4-2-3 ambao ni miaka miwili ya shule ya awali, miaka saba ya shule ya msingi, miaka minne ya sekondari, miaka miwili ya kidato cha tano na sita na miaka mitatu ya chuo (wakati mwingine huzidi kulingana na programu).

Send this to a friend