Asilimia 65 ya wanawake Rwanda wanaamini ni sawa kupigwa na waume zao

0
51

Waziri wa Jinsia na Ukuzaji wa Familia nchini Rwanda, Jeannette Bayisenge, amesema uchunguzi uliofanywa ulibaini kuwa asilimia 65 ya wanawake waliohojiwa walisema ni sawa mwanamke kupigwa na mume wake ikiwa amefanya makosa mbalimbali.

Bayisenge amebainisha kuwa mitazamo hiyo inawapa ugumu zaidi ya kupigana vita dhidi ya ukatili wa kijinsia nchini humo na pia ni dalili tosha kwamba taifa lina kazi kubwa ya kufanya ili kupunguza idadi hiyo.

Mbinu 6 rahisi za kukuwezesha kuweka akiba

Amesema “takriban ya asilimia 18 ya wanawake walisema mke anapaswa kupigwa ikiwa hajapika vizuri na asilimia 31 walisema mke anaweza kupigwa ikiwa amegombana na mumewe.”

“Wakati huo huo asilimia 2 ya wanaume waliohojiwa walikubali mke apigwe ikiwa hajapika vizuri huku asilimia 6 wakisema mke anapaswa kupigwa ikiwa anagombana na mumewe,” amesema.

Ameongeza zaidi kuwa nchi hiyo inahitaji kutumia mikakati mingi zaidi ili kupindua mawazo hayo hasi kwa wananchi wake.

“Kama bado tuna asilimia 65 ya wanawake ambao walisema wanaweza kupigwa chini ya mazingira yaliyotajwa, wanawake hawa wana kazi kubwa ya kuwaelimisha watoto wao,” ameongeza.

Send this to a friend