Asilimia 70 ya wanafunzi wa shule za sekondari wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro hawajui wanataka kuwa nani na wenye taaluma ipi mara baada ya kuhitimu ngazi ya sekondari na vyuo.
Kutokana na hali hiyo, Ofisa Elimu Taaluma Sekondari wa Wilaya hiyo, Emmanuel Kipele amesema kuna haja ya Serikali kutoa elimu ya kujitambua na kujiamini kwa wanafunzi wawapo shuleni pamoja na mafunzo ya stadi za kazi.
Namna 5 ya kuepuka kupatwa na kiharusi
“Wanafunzi wanaohitimu kushindwa kuwa na malengo au ndoto zao, kwamba wanataka kuwa nani, ni jambo ambalo linadidimiza vipaji na kuathiri elimu kwa kuwa na matokeo yasiyoridhisha katika mitihani ya taifa.
“Zamani tulikuwa tukifundishwa namna bora ya kufanya kazi za mikono, na hii ilikuwa inasaidia kuhakikisha mwanafunzi anajitambua na kufahamu kipaji alichonacho,” ameeleza.