Afisa wa serikali nchini India, Rajesh Vishwas ambaye alitoa maji kwenye hifadhi ili kutafuta simu aliyoiangusha wakati akipiga selfie, amesimamishwa kazi.
Inaelezwa kuwa zaidi ya lita milioni 2 za maji zilitolewa nje ya hifadhi ya Paralkot kwa muda wa siku nne katika jitihada za kutafuta simu yake aina ya Samsung.
Imebainika aliyezuia Polisi wasiwakamate watuhumiwa Kisutu ni wakili feki tangu 2019
Katika taarifa iliyotolewa na Indian Express, Vishwas alitoka na marafiki zake katika jimbo la kati la India la Chhattisgarh kisha simu yake iliteleza kutoka mikononi mwake na ndipo alipokodi pampu ya dizeli kutoa maji kwenye mfereji ikiwa ni juhudi za kuitafuta.
Vishwas amedai alifanya hivyo baada ya kuomba ruhusa kutoka kwa afisa wa kitengo kidogo pia aliomba wengine waliokuwa kwenye hifadhi hiyo wajaribu kuitafuta simu hiyo, lakini walishindwa kuipata kwakuwa maji yalikuwa mengi.