Asitisha kugombea ubunge baada ya kupata ajali akienda kuchukua fomu

0
38

Mhadhiri wa Chuo Kikuu Huria Tanzania, Kulwa Mang’ana amepata ajali katika eneo la Boman’gombe wilayani Hai wakati akiwa njiani kuelekea Wilaya ya Siha kwa lengo la kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi.

Kwa mujibu wa mashuhuda, ajali hiyo ilitokea majira ya saa 10:00 jioni njia panda ya kuelekea Siha ambapo dereva wa pikipiki aliigonga gari yake kwenye eneo la mlango wa dereva na kusababisha kuvunjika kwa kioo ambacho vipande vyake vilimuingia sehemu za mwili ikiwemo kichwani.

Baada ya taratibu za kisheria kukamilika katika Kituo Cha Polisi Cha Boma Ng’ombe, Kulwa alieleza kusitisha zoezi la kwenda kuchukua fomu huku akiwatakia kila la kheri wote waliojitokeza kuchukua fomu katika jimbo hilo.

Amesema atasubiri mpaka mwaka 2025, kwa sasa ataendelea kuwa mwanachama mtii, muaminifu na mzalendo kwa nchi yake.

Send this to a friend