Askari ajeruhiwa vibaya na kundi lililojaribu kuvamia mgodi wa North Mara

0
42

Askari wa Jeshi wa Polisi ameripotiwa kujeruhiwa vibaya na kundi la watu waliokuwa wanataka kuvamia Mgodi wa Dhahabu wa North Mara kwa lengo la kupora mawe yenye dhahabu.

Mgodi huo umekuwa ukikabiliwa na uvamizi wa mara kwa mara unaofanywa na makundi ya watu wanaojulikana kama ‘inturders’ ambao hukabiliana mara kadhaa na askari wanaokuwa kwenye doria katika maeneo hayo ya mgodi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Polisi Tarime Rorya, SACP Mark Njera amethibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akibainisha kuwa polisi aliyejeruhiwa ni mwanaume.

Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Mtambi hivi karibuni alifika kutembelea mgodi huo na kutoa wito kwa makundi ya vijana kuacha mara moja vitendo vya kuvamia mgodi huo.

Mgodi wa Dhahabu wa Norh Mara unaendeshwa na Kampuni ya Barrick Gold kwa ubia na Serikali ya Tanzania kupitia Kampuni ya Twiga Minerals.

Send this to a friend