Askari feki akamatwa Buguruni

0
32

Hussein Ramadhan (30) mkazi wa Sinza mkoani Dar es salaam anashikiliwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum baada ya kukutwa amevalia sare za jeshi hilo (jungle Green), akizitumia kukamata  watu na kufanya unyang’anyi wa kutumia nguvu.

Aidha, baada ya kufanyiwa upekuzi wa kina, amekutwa na vifaa vingine kama buti za jeshi la polisi, kadi za benki CRDB, NMB, kadi ya mpigakura na kadi za NSSF zenye jina la Florence Victor Kiondo ambazo zinachungunzwa jinsi alivyozipata na kama zinahusishwa na uhalifu.

Hata hivyo, kumbukumbu zinaonesha kuwa mtuhumiwa huyo anarekodi nyingi za uhalifu kama kujeruhi na kufungwa jela miaka minne katika Magereza ya Mkuza Kibaha, Rwanda, Mbeya na kumalizia kifungo chake gereza la Kitai Mbinga mkoani Ruvuma.

Pia alihukumiwa kifungo cha nje miezi 6 katika Mahakama ya Mwanzo Buguruni kwa  kosa la wizi.

Kamanda wa Polisi Kanda Kaalum ya Dar es salaam, Muliro Jumanne amesema jeshi la polisi litaendelea kuwasaka wale wote wanaotumia sare za jeshi la polisi, na sio askari polisi.

Send this to a friend