Askari wa TANAPA ashikiliwa kwa tuhuma za mauaji ndani ya hifadhi

0
129

Jeshi la Polisi mkoani Katavi linamshikilia Askari wa Hifadhi ya Wanyamapori (TANAPA), Juma Twaha (26) kwa tuhuma za kumpiga risasi na kumuua mtu mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Edga, anayekadiriwa kuwa na miaka 35-40 huko Kijiji cha Ipota, Tarafa ya Mpimbwe, Wilaya ya Mlele mkoani humo.

Taarifa iliyotolewa na Jeshi hilo, imesema Septemba 17, 2025, majira ya saa 10 jioni, Twaha akiwa doria na askari wenzake ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Katavi, waliona watu ndani ya hifadhi hiyo na kujaribu kuwafukuza na ndipo alifyatua risasi na kumpiga Edga kwenye paji la uso na kusababisha kifo chake.

Aidha, Jeshi la Polisi limetoa wito kwa wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi.

Send this to a friend