Askari wanaodaiwa kumuua mlinzi Dar wafukuzwa kazi

0
70

Askari wawili wa Kituo cha Mabatini wanaodaiwa kumuua kwa kumpiga risasi mlinzi wa baa ya Board Room, Riziki Azan wamefukuzwa kazi.

Jeshi la Polidi limesema askari hao wamechukuliwa hatua za kinidhamu huku mmoja akifikishwa mahakamani kwa tuhuma za mauaji.

Azan aliyekuwa mlinzi wa baa iliyoko Sinza, aliuawa usiku wa kuamkia Novemba 29, mwaka huu wakati askari hao wakitaka kumkamata muhudumu wa baa hiyo kwa madai kuwa anafanya biashara ya kujiuza.

Send this to a friend