Askari waonywa kushabikia vyama vya siasa

0
43

Kamanda wa Polisi Kikosi cha Kuzuia Wizi wa Mifugo Nchini, Kamishina Msaidizi wa Polisi, ACP Simon Pasua amewataka askari wa Jeshi la Polisi mkoani Arusha kutojihusisha na ushabiki wa vyama vya siasa badala yake kujikita katika ulinzi na usalama wa raia na mali zao.

ACP Pasua ameyasema hayo leo wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza askari waliofanya vizur zaidi mwaka jana 2022 mkoani Arusha na kubainisha kuwa askari wanapaswa kushabikia masuala mengine ya kijamiii kama vile michezo na kuwataka kujikita zaidi katika ulinzi wa raia na mali zao ili kuleta ufanisi na kupunguza manung’uniko ya wananchi.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishina Msaidizi wa Polisi, ACP Justine Masejo amempongeza kamanda wa kikosi hicho kwa kutambua mchango wa askari wanaofanya kazi vizuri zaidi kazini na kuongeza kuwa Watanzania wanalitegemea sana jeshi hilo.

Naye askari wa kikosi hicho kutoka Koplo wa Polisi, Silvester Mang’aha ambaye amepata zawadi kwa kufanya kazi vizuri mwaka 2022 amewashukuru askari wenzake na kubainisha kuwa kitendo cha kupata zawadi hiyo ni kutokana na mchango na ushirikiano kutoka kwa askari wenzake.

Send this to a friend