Askari watatu, mgambo mbaroni kwa mauaji Tabora

0
26

Jeshi la Polisi mkoani Tabora linawashikilia askari watatu wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) pamoja na mgambo wanne kwa tuhuma za kusababisha kifo cha Grace Mussa (04) mwanafunzi wa elimu ya awali, na kumjeruhi Zengo Sandu (47) kwa risasi katika Kijiji cha Igwisi, Tarafa ya Kazaroho wilayani Kaliua.

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Richard Abwao amesema tukio hilo limetokea Desemba 2, mwaka huu ambapo askari wa TFS wakiwa kwenye doria katika Hifadhi ya Msitu wa Taifa Kigosi Moyowosi, walikamata trekta lenye namba za usajili T 689 DCA, mali ya Sandu Kate ambalo lilikuwa likilima ndani ya hifadhi.

Polisi: Taarifa kuhusu viongozi wa upinzani kufanyiwa uhalifu ni za kutengeneza

Ameongeza kuwa wakiwa njiani kurudi kambini eneo la Igombambili, Kitongoji cha Mpanda Mlowoka, wananchi walijikusanya na kuwazuia askari hao wasipeleke trekta hilo kambini, ndipo askari hao walifyatua risasi na kusababisha kifo cha mtoto huyo na kumjeruhi mmoja kwenye mkono wa kushoto.

Jeshi la Polisi limesema uchunguzi wa daktari umeeleza kuwa chanzo cha kifo cha mtoto huyo ni kuvuja kwa damu nyingi.

Send this to a friend