Askari wawili wakamatwa Dar sakata la kifo cha mlinzi wa baa

0
47

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata askari polisi wawili kwa kosa la kumjeruhi kwa risasi mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Razaki Azan (29) ambaye baadaye alipoteza maisha.

Kaimu Kamanda Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Gabriel Puppa amesema marehemu ambaye alikuwa mlinzi binafsi wa baa inayojulikana kama Boardroom alifanyiwa tukio hilo usiku Novemba 29, 2023 katika eneo la Sinza Mapambano, Kinondoni mkoani Dar es Salaam.

“Jeshi la Polisi tayari limewakamata askari hao na mambo ya kisheria yanakamilishwa na watachukuliwa hatua za kisheria haraka kadri iwezekanavyo kwa kufuata mifumo ya kisheria ikiwa ni pamoja na kuwafikisha mahakamani,” ameeleza.

Kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi la Polisi, mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Rufaa Mwananyamala kwa ajili ya kukamilisha uchunguzi.

Send this to a friend