Askofu adaiwa kujinyonga kisa madeni

0
47

Katika hali isiyo ya kawaidia, Askofu Mkuu wa Makanisa ya Methodist Tanzania, Askofu Joseph Bundala (55) amekutwa amejinyonga katika ofisi za kanisa hilo lililopo mtaa wa Sulungai Meriwa Kata ya Ipagala jijini Dodoma kwa kutumia waya wa simu akidai chanzo ni madeni.

Tukio hilo limetokea Mei 16, mwaka huu kwenye choo cha ofisi yake ambapo umekutwa waraka unaodaiwa kuandikwa na marehemu kabla ya kuchukua uamuzi huo unaodai kuwa chanzo cha kufanya hivyo ni kutokana na mgogoro wa madeni ambayo hakubainisha kiasi cha fedha.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani humo, Alchelaus Mutalemwa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa uchunguzi wa kina unaendelea juu ya tukio hilo.

“Uchunguzi katika eneo la tukio umekuta ujumbe unaeleza sababu za kujinyonga ni madeni na mgogoro uliopo kati ya uendeshaji wa shule binafsi. Uchunguzi bado unaendelea,” amesema Kamanda.

Send this to a friend