Aslay ataja kilichosababisha apotee kwenye muziki

0
58

Msanii wa muziki Tanzania, Aslay Isihaka kwa mara ya kwanza ameweka wazi mambo yaliyomfanya apotee kwenye tasnia ya muziki huku akitaja kifo cha mama yake pamoja na kuachana na mama wa mtoto wake kuwa chanzo cha kuyumba katika tasnia hiyo.

Katika filamu yake aliyoipa jina la ‘Mimi ni Bongo Fleva’ Aslay amedai alipatwa na msongo wa mawazo baada ya kutaarifiwa kifo cha mama yake aliyefariki usiku akiwa anatumbuiza kisha kupewa habari hizo asubuhi.

Aidha, ameeleza kuwa baada ya kusambaratika kwa kundi la muziki la Yamoto Band ambalo alikuwa mmoja wa wasanii walioonekana kupendwa zaidi, watu wengi walimfuata kufanya naye kazi  zikiwemo lebo kubwa za Tanzania.

Vigezo 10 vinavyoangaliwa zaidi na wanaume kwa wanawake wanapotaka kuoa

“Lebo kubwa tatu zilinifuata  ili kufanya nao kazi, siwezi kuzitaja ila kila moja ilikuja kwa njia yake,” amesema Aslay.

Ameongeza, “lebo ya kwanza ilikuja, walivyonielezea sikupendezewa na mikataba yao jinsi walivyotaka, kwa sababu mimi ni mtu ambaye napenda sana kujiamini kwahiyo sipendi sana kubanwa kwenye kazi zangu hivyo nilishindwa kusaini.”

Send this to a friend