Atapeliwa na kaka yake aliyekuwa akimtumia pesa kwa miaka 15 amjengee nyumba

0
47

Mwanamke mmoja raia wa Nigeria amejikuta akimwaga machozi kwa uchungu baada ya kurejea nchini humo kutoka ughaibuni alipokuwa akifanya kazi na kubaini kaka yake alikuwa akimtapeli kwa kudhani alikuwa akimjengea nyumba kwa pesa alizokuwa akimtumia.

Mwanamke huyo ambaye amekuwa akimtumia kaka yake pesa kwa takribani miaka 15, alipatwa na mshtuko mkubwa baada ya kujua pesa alizokuwa akituma zimeelekezwa kwenye matumizi mengine na hakuna nyumba iliyojengwa.

Picha na video zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zinamwonesha mwanamke huyo akijiviringisha kwenye tope huku akilia kwa uchungu kwa upotevu wa pesa zake.

Tukio hilo limezua hisia kubwa katika mitandao ya kijamii huku wengine wakishauri kwa wanaofanya kazi nje ya nchi kutoamini watu na kutunza pesa zao wenyewe pasipo kuwategemea wanafamilia kwa ajili ya uwekezaji wowote.

Send this to a friend