Atayeleta vifaa kinga vya corona visivyo salama kushtakiwa kwa mauaji

0
37

Katika kuendelea kukabiliana na maambukizi ya virusi vya corona, Rais Dkt Magufuli amewataka watu wote wanaopokea misaada ya vifaa mbalimbali kwa ajili ya kujikinga na corona kuhakikisha kuwa vinakuwa salama, na vinapitia kwanza wizara ya afya.

Rais amesema hilo na kuongeza kuwa wizara ya afya ina wataalam ambao watavikagua vifaa hivyo kujua kama ni salama kwa matumizi, kutokana na kile alichosema kuwa, vita ya corona ni sawa na vita nyingine.

“Na kwa mtu yeyote atakayepewa mavifaa ya kuzuia corona, halafu mkayapima mkayakuta yana corona, huyo mtu apelekwe kwenye kesi ya jinai, hata ya mauaji kama wauaji wengine,” amesisitiza.

Aidha, amewataka watendaji kujiepusha kupokea pokea misaada, huku akisema kama kuna nchi au taasisi inataka kutoa msaada, itoe fedha, kisha serikali itanunua vifaa ambavyo inaamini ni salama.

Katika hilo hilo, amezipongeza taasisi mbalimbali ikiwamo Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kutokana na kutengeneza vifaa kinga vikiwamo barakoa na mavazi binafsi ya kujikinga (PPE) ambavyo vyote vinapatikana kwa bei nafuu.

Send this to a friend