ATCL: Boeng 787-7 (Dreamliner) mbili zipo kwenye matengenezo

0
51

Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) imesema imesitisha safari zake kwenda Guangzhou, China kutokana na ndege zake mbili za masafa marefu aina ya Boeng 787-7 (Dreamliner) kufikia muda wake wa matengenezo ya kawaida (maintainance schedule) ambayo yalishindwa kufanyika kwa awamu kutokana na athari za UVIKO-19.

Kwa mujibu wa taarifa ya ATCL imesema utaratibu wa matengenezo haukufanyika kutokana na kuvurugika kwa mfumo wa ugavi (supply chain) katika utengenezaji wa vipuri vya ndege uliosababishwa na athari za janga hilo.

“Ratiba ya matengenezo ya kawaida kwa ndege zetu zote za Boeng 787-7 (Dreamliner) imepangwa kufanyika kwa pamoja ili kuondoa hatari ya kukosekana kwake kwa muda mrefu ikiwa tutapoteza nafasi ya matengenezo tuliyopangiwa. Huu ni utaratibu wa kawaida kwa mashirika yote ya ndege duniani,” imesema ATCL.

Sababu 7 zinazoweza kupelekea kunyimwa visa

Aidha, ATCL imesema kuna utaratibu maalum ulioandaliwa kwa abiria wote wa safari za Guangzhou ili safari zao ziendelee kama kawaida, kama walivyofahamishwa hapo awali.

Kwa mujibu wa ATCL katika mahojiano na Swahili Times, kampuni hiyo imesitisha safari hizo hadi Oktoba 16, mwaka huu

Send this to a friend