ATCL kuingia makubaliano na Emirates na KLM

0
55
Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) ipo katika hatua za mwisho za kuingia makubaliano ya ushirikiano na mashirika ya Emirates na KLM ambayo yatawezesha kubadilishana abiria Marekani na Ulaya.
 
Aidha, kampuni hiyo imeeleza kwamba ipo katika hatua za mwizo za mazungumzio na Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya China kwa ajili ya ushirikiano sawa na huo.
 
“Haya ni makampuni makubwa duniani. Kama njia ya kukuza safari zetu, tunaanza na ushirikiano nao wakati tukijiandaa kwenda Ulaya na Marekani, amesema Mkurugenzi Mkuu wa ATCL, Ladislaus Matindi.
Send this to a friend