ATCL kupunguza na kufuta baadhi ya safari zake

0
93

Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) imesema itapunguza miruko na kufuta baadhi ya safari zake kulingana na idadi ya ndege zilizopo ili kutoa muda kwa watengenezaji wa injini kushughulikia matatizo yaliyopo.

ATCL imesema mabadiliko hayo ya muda mfupi ni kutokana na changamoto za kiufundi kote duniani za injini aina ya PW1524G-3 zinazotumika katika ndege za Airbus A220-300.

Shujaa Majaliwa aanza mafunzo chuo cha Zimamoto Tanga

“Kwa kuzingatia matakwa ya usalama, tumekuwa tukifuata maelekezo ya kitaalam ili kutoa huduma bora na ya usalama. Na wakati mwingine tunazitoa ndege katika mzunguko kukidhi matakwa ya watengenezaji wa injini hizi.

“Hatua hizi zimesababisha ucheleweshaji wa ndege zetu wakati changamoto hii ikitafutiwa ufumbuzi,” imeeleza kampuni hiyo katika taarifa yake kwa umma.

Send this to a friend