ATCL leo imezindua safari za ndege kwenda mkoani Geita

0
58

KAMPUNI ya Ndege Tanzania (ATCL) leo Januari 9, 2021 imezindua safari safari za ndege kwenda mkoani Geita.

Hayo yamesema na Mtendaji Mkuu wa ATCL, Mhandishi Ladislaus Matindi wakati akiwa katika Uwanja wa Ndege wa Mkoa wa Geita uliopo wilayani Chato ambapo amesema kwa kuanza wataanza na safari mbili kwa wiki.

Matindi amesema safari hizo za kwenda Geita kutokea Dar es Salaama na Geita kwenda Dar es Salaam zitakuwa Alhamisi na Jumamosi.

Aidha, amesema kuanzia Januari 18, 2021 safari hizo zitaongezwa kuwa tatu kwa wiki, zitakazokuwa siku za Jumatatu, Alhamisi na Jumamosi.

Mapema mwezi huu Mkuu wa Mkoa wa Geita, Robert Gavriel alisema kuanza kwa safari za ndege mkoani humo kutasaidia kusafirisha kwa urahisi watalii wanaotembelea mbuga za wanyama Burigi-Chato na Visiwa vya Hifadhi ya Rubondo na pia safari hizo zitasaidia kukuza sekta za madini, uvuvi, kilimo na biashara.

Uwanja huo wa ndege wenye urefu wa kilomita sita na upana wa kilomita moja umegharimu zaidi ya TZS 58 bilioni ambazo ni fedha zinazotokana na mapato ya ndani.

Send this to a friend