ATCL yasitisha safari kwenda China 

0
78

Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) imesema imesitisha safari za Tanzania kwenda Guangzhou nchini China hadi Oktoba 16 mwaka huu kutokana na suala la kiufundi.

Akizungumza na Swahili Times, Anna Paul kutoka kituo cha mawasiliano na huduma kwa wateja amesema wateja waliokwisha kata tiketi zao watasafiri kupitia Shirika la Ndege la Qatar.

Safari za ndege za abiria kutoka Tanzania kwenda Guangzhou, China zilirejea rasmi Julai 17, 2022 baada ya kusitishwa kwa muda kutokana na janga la UVIKO- 19 ambalo liliibuka mwishoni mwa mwak 2019 na kuleta athari kubwa ulimwenguni ikiwemo vifo.

China na Tanzania ni washirika wazuri wa kibiashara. Pia nchi hiyo imekuwa na mchango mkubwa katika uchumi wa Tanzania ikiwemo kuboresha miundombinu ya usafirishaji.

China imechangia kwa kiasi kikubwa katika kufadhili na kutekeleza miradi mikubwa ya miundombinu nchini Tanzania, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa barabara, madaraja, reli na viwanja vya ndege.

Send this to a friend