ATCL yatangaza mabadiliko ya ratiba kutokana na uchache wa ndege

0
34

Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL) imesema inapitia changamoto za mabadiliko ya ratiba za ndege kutokana na uchache wa ndege zilizobaki iliosababishwa na kuchelewa kwa upatikanaji wa injini mbadala za ndege mbili zenye matatizo ya injini.

Kampuni hiyo imesema injini mbadala za ndege hizo aina ya Airbus A 220-300 zinazotakiwa kutolewa na na mtengenezaji Pretty & Whitney (P&W) zilitarajiwa kuwasili mwanzoni mwa mwezi Aprili mwaka huu.

Maharage: Vyura 12,000 wamesharejeshwa nchini kutoka Marekani

“Kutokana na changamoto hizi tunalazimika kutoa huduma kwa ratiba inayobanana sana ili kukidhi mahitaji makubwa ya wateja wetu. Wakati tunashughulikia changamoto hizi kwa haraka, tunaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza,” imesema katika taarifa.

Aidha, Kampuni imesema itaendelea kuhakikisha inatoa hudumaa bora ili kufikia matarajio ya wateja wao.

Send this to a friend