ATCL yazindua ulipaji wa nauli kidogo kidogo (Kibubu)

0
61

Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL) imeanzisha uataratibu wa kulipia nauli kwa njia ya ‘Kibubu,’ ambapo mwananchi atalipa nauli kidogo kidogo hadi kukamilisha nauli inayotakiwa.

“Sasa unaweza kupanga safari yako mapema na kulipia tiketi yako kidogo kidogo hadi wiki moja kabla ya safari yako. Hii huduma ni kwa wateja wetu wote na ni kwa safari zetu zote za ndani na nje ya nchi,” imeeleza kampuni hiyo.

Kupitia kibubu mwananchi atatakiwa kuweka TZS 50,000 kwa mara ya kwanza na kiasi kinachobakia atatakiwa kulipa kidogo kidogo kwa kiwango anachokimudu mpaka safari yake itakapofika.

Kampuni hiyo imesisitiza kwamba huduma ya kibubu inapatikana kwenye ofisi za shirika hilo tu na kwamba vigezo na masharti vitazingatiwa.

Send this to a friend