Ateketeza majengo ya mwajiri wake na kufariki baada ya kufukuzwa kazi

0
80

Mwanaume mwenye umri wa miaka 36 amejiua katika eneo la Mwatungo, Masinga nchini Kenya baada ya kutofautiana na mwajiri wake.

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Polisi nchini humo, mwanaume huyo ambaye alikuwa mfugaji katika nyumba hiyo, alifukuzwa kazi hivi karibuni kutoka kwenye nyumba aliyokuwa akifanya kazi kwa muda.

Ripoti imeeleza kuwa baada ya kufutwa kazi, alirudi kwenye nyumba hiyo na kuchoma trekta, ghala la nyasi, na majengo mengine ndani ya eneo hilo kisha na yeye kupoteza maisha yake kufuatia moto huo.

Mwili wa mfugaji huyo ulipatikana baadaye ukining’inia kutoka kwenye moja ya miti ya eneo hilo.

Maafisa wa polisi kutoka kituo cha polisi cha Kithyoko wamesema kwasasa wanaendelea kuchunguza tukio hilo ili kubaini hasa chanzo cha mzozo huo kilichosababisha mwanaume huyo kuchukua uamuzi huo wa kikatili.

Send this to a friend