Athari 5 za kujinyima kula usizozifahamu

0
15

Ni jambo la kawaida kwa watu wengi kukaa muda mrefu bila kula huku wakidai wanafanya ‘diet.’
Kwa mujibu wa Ofisa lishe, Johari Matiko kutoka hospitali ya Taifa ya Muhimbili anaeleza athari za kuacha kula kwa lengo la kupunguza mwili.

Kushuka kwa kinga ya mwili
Mwili hukosa vyakula muhimu vyenye virutubishi vya kujenga mwili na kusababisha kinga ya mwili kushuka. Kinga ya mwili inaposhuka hukuweka kwenye hatari ya kuambukizwa magonjwa.

Kuvunjika kwa mifupa
Kwa mujibu wa Johari, kujinyima kula pia husababisha madini ya kalsiamu kupungua mwilini, hivyo mifupa ya mhusika huwa rahisi kuvunjika na kupata matatizo ya gauti.

Vidonda vya tumbo
Unaweza kupata vidonda vya tumbo kutokana na utumbo kukaa muda mrefu bila chakula. Mazingira ya umeng’enyaji chakula huandaliwa ambapo tindikali humwagwa tumboni kwaajili ya kuchakata chakula.

Tatizo kwenye ubongo
Inaelezwa kuwa unapoacha kula hutokea tatizo la vichocheo kushindwa kuwa sawa na kutengeneza tatizo kwenye ubongo. Ili ubongo ufanye kazi unahitaji chakula, ukikaa muda mrefu bila kula kichwa hushindwa kufanya kazi vizuri.

Matatizo ya tumbo na choo
Unaweza kupitia maumivu ya tumbo kutokana na kutokula kwa wakati, pia kupata matatizo mbalimbali ikiwemo kupata choo kigumu.

Nini cha kufanya ili kupunguza mwili bila madhara?
Unashauriwa njia sahihi ya kupunguza mwili ni kufanya mazoezi na kupunguza kiwango cha wanga (mfano ugali, wali, chapati, sukari na mafuta) kwenye mlo wako wa kila siku.
Upande wa matunda pia, unashauriwa kuepuka matunda yenye wingi wa sukari na badala yake tumia zaidi yenye nyuzinyuzi.

Chanzo: Mwananchi

Send this to a friend