Athari 5 za kuvaa Earphones kwa muda mrefu

0
68

Ni jambo la kawaida kumkuta mtu ameweka masikioni vipokea sauti masikioni(EarPhones) huku akiendelea na shughuli zake. Vifaa hivi vimekua kama msaada wa kukamilisha shughuli flani kwa baadhi ya watu hasa vijana kwani unaweza kukua amevaa huku akiwa anasoma, anaosha vyombo, anapika na wengine wakiwa kwenye mazoezi.

Lakini ukweli ni kwamba hakuna kizuri kisicho na ubaya, vipokea sauti hivi vinapotumika kwa muda mrefu na kwa sauti ya juu zaidi basi zinaweza kukuletea madhara ya kiafya kadri muda unavyozidi kwenda.

Utafiti uliofanywa na Dk. Amarjeet Bhatia umegundua madhara yafuatayo yanayotokana na uvaaji vipokea sauti kwa muda mrefu.

1. Tatizo la kusikia
Unapovaa vipokea sauti vya masikioni kwa muda mrefu na kusikiliza muziki kwa sauti ya juu sana, basi unaharibu ngoma zako za masikio yako. Sauti inapukua juu ya kiwango kinachohitajika ni hatari hivyo inaweza kukusababishia tatizo la kutosikia.

2. Husababisha ubadilishanaji wa vijidudu
Je, unatambua kwamba kubadilishana earphones ina maana pia kubadilishana vijidudu na uwezekano wa maambukizi ya sikio na mtu? Ni muhimu kusafisha vipokea sauti vya masikioni unapobadilishana na mtu.

3. Kutosafisha earphone zako mwenyewe
Ikiwa huna tabia ya kusafisha earphone zako mara kwa mara, baada ya muda huanza kujilimbikiza kila aina ya vijidudu na kusababisha maambukizi kwenye sikio lako.

4. Maumivu ya sikio na Kizunguzungu
Unapaswa kupunguza matumizi yako, kwani kelele kubwa inaweza kusababisha shinikizo kwenye mfereji wa sikio, hivyo itakufanya uhisi kizunguzungu. Ikiwa unatumia earphone zilizowekwa vibaya, basi unaweza kutengeneza tatizo na kusababisha maumivu kwenye sikio lako la ndani.

5. Kutofahamu ulimwengu wa nje
Masikio yako ni chombo muhimu cha hisia. Hukusaidia kuelewa vizuri mazingira ya nje, ikiwa unatumia earphones unapokuwa barabarani una uwezekano mkubwa wa kupata ajali kwani uwezo wako wa kusikia haufanyi kazi.
Matumizi ya earphone haipaswi kuzidi saa moja kwa siku. Hakikisha unapunguza matumizi yako na kuzuia maumivu ya sikio au upotevu wa kusikia.

Send this to a friend