Wafanyakazi wengi ofisini hutumia zaidi ya saa sita kukaa chini kila siku. Mbali na kupata maumivu mara kadhaa ya mgongo, pia kuketi kunaweza kusababisha athari za muda mrefu kwa afya na mwili wako.
Hizi ni baadhi ya athari zinazoweza kujitokeza unapoketi kwa muda mrefu;
Kuongeza Uzito
Kushughulisha mwili husababisha misuli yako kutoa molekuli kama lipoprotein lipase ambayo husaidia kusindika mafuta na sukari unayokula. Unapotumia zaidi ya siku yako umekaa, kutolewa kwa molekuli hizi hupunguzwa na unakuwa katika hatari kubwa ya kupata ugonjwa wa kimetaboliki, hata kama unafanya mazoezi.
Kuharibu mgongo na maumivu
Kukaa inaweza pia kuumiza mgongo wako haswa ikiwa una mkao mbaya au hutumii kiti cha ergonomic. Pia mkao mbaya unaweza kusababisha ukandamizaji kwenye diski kwenye mgongo wako na kusababisha kuharibika pamoja na maumivu ya muda mrefu.
Aina 5 ya vyakula ambavyo vikichanganywa hugeuka sumu
Athari za kiakili
Kukaa kwa muda mrefu kunaweza kuchangia wasiwasi. Hii ni kwa sababu mwili na akili viko sehemu moja pekee siku nzima tofauti na mtu anayeshughulisha mwili na kukutana na vitu tofauti tofauti. Hatari hizi zinaweza kupunguzwa kwa mazoezi ya kawaida.
Hatari ya Saratani
Uchunguzi unaonesha kuwa kukaa kwa muda mrefu kunaweza kuongeza hatari ya aina fulani za saratani ikiwemo saratani ya mapafu, uterasi na utumbo.
Ugonjwa wa Moyo
Kuketi kunaweza kusababisha ugonjwa wa moyo na mishipa. Wataalamu wanasema watu wanaokaa zaidi wana hatari kubwa ya asilimia 147 ya kukumbwa na mshtuko wa moyo au kiharusi.
Hatari ya Kisukari
Watafiti wanaeleza kuwa watu wanaotumia muda mwingi kukaa pia wana asilimia 112 ya hatari ya kupata ugonjwa wa kisukari.
Deep Vein Thrombosis (DVT)
Hii ni aina ya kuganda kwa damu ambayo hupatikana sana kwenye miguu. Sehemu ya donge hili inapopasuka inaweza kukata mtiririko wa damu kwenda sehemu nyingine za mwili kama vile mapafu yako na kusababisha mshipa wa mapafu. Hali hii inaweza kusababisha kifo. Kukaa kwa muda mrefu sana hata kwenye safari ndefu ya barabarani, kunaweza kusababisha DVT.