Athari za kiafya za ubandikaji kucha bandia

0
101

Urembo wa kubandika kucha umeshamiri sana hivi sasa hasa kwa mabinti na wanawake wa rika tofauti.

Lakini licha ya urembo huu kupendwa na wengi, wataalam wa afya wanasema umekuwa ukisababisha athari kwa watumiaji wake  kutokana na kutumika kwa gundi ambazo hunata kwenye ngozi.

Haya ni baadhi ya madhara ambayo yametajwa kuchangiwa na ubandikaji wa kucha bandia.

Uvimbe
Kemikali zinazotumiwa kupachika au kuondoa kucha za bandia zinaweza kuwasha ngozi yako, unaweza kuona uwekundu, usaha, au uvimbe kwenye kucha zako, zinaweza kuwa na ‘resini’na ‘formaldehyde’ ambazo zimehusishwa na saratani ambao unaweza kusababisha uharibifu wa kucha.

Mambo 5 yanayoweza kutokea unapotumia simu wakati unaichaji

Kuathiri ukuaji wa kucha
Matumizi ya mara kwa mara ya kucha bandia yanaweza kuathiri ukuaji wa kucha na kuifanya iwe rahisi kuvunjika, pia hukausha mafuta ya asili kwenye kucha zako na kuzifanya ziwe rahisi kugawanyika.

Ugonjwa wa eczema
Kemikali zinazotumiwa kubandika kucha baadhi hazina ubora na kusababisha kupata ugonjwa wa ngozi ambao ni aina ya eczema. Hii inaweza kuchangiwa na  kucha bandia yenyewe au gundi ambayo hutumiwa kuiunganisha.

Dalili za eczema zinaweza kujumuisha sio tu maumivu, bali pia;
•Uwekundu au kubadilika rangi
•Kuwashwa
•Mabaka yaliyopasuka au magamba
•Ukavu

Nini unaweza kufanya ili kuzuia madhara hayo?

Ikiwa unapenda kuonekana na kucha bandia, vidokezo hivi vinaweza kukusaidia kukuweka salama.

Sitisha kubandika kucha za bandia kila baada ya miezi kadhaa ili kuruhusu kucha zako halisi kupumua kutokana na kemikali.

Chagua saluni ambayo huimarisha rangi ya ‘gel’ kwa taa za ‘LED’ ambazo zina kiasi kidogo cha mwanga wa ‘UV’.

Usikae na kucha bandia kwa zaidi ya wiki mbili ili kuepuka uharibifu kwenye kucha  pamoja na ngozi yako.

Unashauriwa kuweka kucha bandia katika matukio maalum ili kupunguza hatari ya uharibifu wa kucha zako.

Send this to a friend