Atibiwa bure baada ya kudanganywa kuwa ni Makamu wa Rais

0
40

Mwanaume mmoja nchini Zimbabwe amepandishwa kizimbani kwa tuhuma za ulaghai baada ya kudanganya kuwa ni Makamu wa Rais wa nchi hiyo ili apate matibabu bure hospitalini.

Mahakama katika Mji Mkuu wa Harare imesikiliza kesi hiyo ambapo Marlon Katiyo (35) alitembelea hospitali mbili kwa nyakati tofauti mwezi uliopita kwa ajili ya kupata matibabu ya kichwa na kusema kuwa ni Makamu wa Rais, Constantino Chiwenga..

Udanganyifu huo ulimwezesha Katiyo kupata matibabu ya bure.

Hata hivyo hajasema chochote katika kesi hiyo ya kujifanya Chiwenga mwenye umri wa miaka 65.

Uamuzi kuhusu maombi yake ya dhamana unatarajiwa kutolewa leo nchini humo.

Send this to a friend