Mwanaume mwenye umri wa miaka 24, anayejulikana kwa jina Anthony Ouma, ameuawa na mashabiki wenye hasira katika klabu ya usiku mjini Bondo nchini Kenya majira ya alfajiri ya Siku ya Kupeana Zawadi (Boxing Day).
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Wilaya Ndogo ya Bondo, Robert Aboki, Ouma alihudhuria tamasha la muziki la Krismasi katika kilabu hiyo, ambapo alidaiwa kumshambulia msanii aliyekuwa akitumbuiza, Odongo Swag akijaribu zinasema kwamba Ouma alijaribu kumpiga msanii huyo kichwani kwa chupa wakati wa onyesho hilo.
Mashabiki waliokuwa wamehudhuria tamasha hilo walimshambulia kwa mateke, ngumi, na silaha za kienyeji, na kusababisha kifo chake.
Aboki amethibitisha tukio hilo, lililotokea saa kumi na moja alfajiri, na kusema kuwa mwili wa marehemu uliondolewa na polisi na kupelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya wilaya ndogo ya Bondo kusubiri uchunguzi wa mwili (postmortem).