Auawa na Polisi kwa kuwashambulia kwa mishale yenye sumu

0
36

Mkazi wa kijiji cha Chioli, kata ya Songolo wilayani Chemba, Mkoa wa Dodoma, Nada Songo (45), ameuawa na Jeshi la Polisi akidaiwa kuwashambulia askari na wananchi kwa mishale yenye sumu.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma, Martin Otieno amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema Jumapili Agosti 28 mtuhumiwa huyo alifanya matukio hayo katika kijiji cha Chioli.

Watoto wanne wafariki baada ya mganga kuwasha moto kufukuza mikosi

Ameongeza kuwa mtuhumiwa huyo amefariki mara baada ya kupigwa risasi na askari maeneo ya kifuani na mguu wa kulia wakati akiwashambulia askari hao kwa mishale inayodhaniwa kuwa na sumu.

Aidha, Kamanda Otieno amesema Agosti 27, 2022 mtuhumiwa aliwashambulia wanakijiji kwa kuwatishia kwa mishale yenye sumu.

Send this to a friend