Avunjwa miguu na kiuno na Mkuu wa Kituo cha Polisi kwa kutembea na mke wake

0
96

Askari Polisi ambaye pia ni Mkuu wa Kituo kidogo cha Polisi Kiseke kilichopo Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza a anatafutwa na Jeshi la Polisi baada ya kudaiwa kumvunja miguu na kiuno, Mohammed Khatibu (29) kwa tuhuma za kuwa na mahusiano na mke wake.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani humo, Gedion Msuya amethibitisha kutokea kwa tukio hilo  ambalo limetokea Januari 3, mwaka huu kilichofanywa na Mkuu huyo wa kituo, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Paulo anayedaiwa kushirikiana na rafiki yake kufanya tukio hilo.

Imeelezwa kuwa siku ya tukio hilo askari huyo pamoja na rafiki yake walifika nyumbani kwa Khatibu wakitumia gari binafsi kisha kumkamata bila kumweleza kosa lake na kudai wanampeleka Kituo cha Polisi Kirumba ambako ndugu zake walimkosa mara walipomfuatilia huko.

“Tulikipita kituo hicho na wakanipeleka Kituo cha Polisi Kiseke. Nilipofikishwa pale kitioni nilifungwa kitambaa cheusi na pingu mikononi  na kuanza kushushiwa kipigo, ndipo nikapelekwa mahabusu bila taarifa zangu kuandikishwa,” ameeleza.

Ameeleza  alipigwa vikali akihojiwa ni kwanini anatembea na mke wa Mkuu wa Kituo na kupelekea kuvunjwa miguu na majeraha kwenye uti wa mgongo.

Chanzo: Mwananchi

Send this to a friend