Baada ya miaka 43 madarakani, Rais wa Equatorial Guinea kugombea tena

0
21

Rais wa Equatorial Guinea, Teodoro Obiang Nguema Mbasogo ambaye ameiongoza nchi hiyo kwa miaka 43, amethibitisha kuwa atagombea tena katika uchaguzi wa Novemba.

Mtoto wake ambaye pia ni Makamu wa Rais, Teodoro Nguema Obiang Mangue, ametoa tangazo hilo kupitia ukurasa wa Twitter siku ya Ijumaa akisema ni “Kwa sababu ya haiba yake, uongozi wake na uzoefu wake wa kisiasa.”

Mashirika ya kutetea haki na mataifa ya kigeni yanasema kuwa utawala wa Obiang umekuwa na mateso kwa wapinzani wa kisiasa, wenye chaguzi za udanganyifu na ufisadi, lakini Obiang anakanusha mashtaka hayo.

Inadaiwa kuwa, mapato ya nchi hiyo ya Afrika Magharibi inayotegemea mafuta na gesi, ambayo ni karibu asilimia 75 ya mapato huwafaidisha walio karibu na Rais huku wengi katika taifa hilo wakiishi katika umaskini.

Chama cha Obiang cha Democratic Party of Equatorial Guinea kinashikilia viti 99 kati ya 100 katika bunge linalomaliza muda wake, na viti vyote 70 ni vya seneti.